Breaking News

KWANINI NAPE NNAUYE AMESHIKA VICHWA VYA HABARI.JICHO KATIKA HABARI STAR TV

Tukio la kutenguliwa na kutoka katika nafasi yake aliyekuwa waziri wa habari ,michezo na utamaduni NAPE NNAUYE limekuwa na taswira nyingi sana hasa alipozuiliwa asifanye mkutano wake na waandishi wa habari hapo jana na kufikia kuoneshewa bastola, ingawaje baada ya hapo alisisitiza watu watambue kuwa NAPE ni mdogo kuliko nchi yetu kubwa ya taifa letu la Tanzania hivyo watanzania wanapaswa kuheshimu uamuzi wa Raisi kwani hakufanya vibaya kumchagua mh.MWAKYEMBE kukaimu nafasi hiyo.


Picha na video za tukio lile zilisambaa kwa kasi sana na kukamata masikio ya watanzania wengi sana kwa muda mfupi na kusababisha gumzo kubwa katika mahala watu wanamoishi jambo ambalo limepelekea hata habari ya Raisi kufanya ziara yake Bandarini hapo jana na kubaini udanganyifu wa kupitisha vitu ikawa haikuonekana kufuatiliwa sana na watanzania wakati lile lilikuwa ni jambo la kimaendeleo, nina hakika Raisi hakujisikia vizuri hata kidogo kwa kuwa alifanya jambo lenye tija kwa taifa.


Karibuni raisi alisisitiza raia wote hasa watumia mitandao kuwa wanatakiwa kufuatilia mambo na habari zenye tija kwa taifa, msisitizo huo ukazua mijadala mingi sana na wengi kufungua vinywa kuzungumza kuhusu vyombo vya habari na tasnia ya habari.


Sikiliza mazungumzo yaliyofanywa katika kituo cha runinga chaStar TV asubuhi hii katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.. ambayo yalizungumzwa mengi sana.







Ambapo pia amelizungumzia sana kuhusu kuwa na strong media,, yaani chombo cha habari madhubuti ambavyo vitasimama na kusema kweli bila upendeleo wala kushinikizwa na watu fulani,

pia waandishi waache kukuza habari kwa kuangalia namna wanavyoandika vichwa vya habari.



Mwisho wakayazumza haya kuhitimisha.



Mungu ibariki nchi yetu isonge mbele.

No comments